Ripoti ya ABNA- Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Moualem amesema serikali yake inashangazwa na hatua hiyo ya Marekani ya kuunga mkono makundi ya kigaidi nchini mwake huku akisisitiza kuwa serikali yake iko tayari kwa mazungumzo ya kisiasa ili kumaliza mapigano yanayoendelea.Mualem amewaambia wajumbe katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kuwa nchi yake imekuwa ikikabiliana na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni tangu kuanza kwa mapambano nchini mwake mwaka uliopita.Marekani na Ufaransa zaendelea kusisitiza mabadiliko nchini Syria huku Qatar, Saudi Arabia na Uturuki kuhami waasi hao kwa silaha na fedha.Mashambulizi yanayoongozwa na majeshi ya Syria yameendelea kuwashambulia waasi katika mji wa Allepo na kusababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia wakiwemo watoto.Mapigano dhidi ya Serikali ya Syria yameingia katika mwezi wa kumi na tisa
1 Oktoba 2012 - 20:30
Msimbo wa Habari: 352899
Serikali ya Syria imeeleza kuwa Marekani pamoja na washirika wake ndio waunga mkono ugaidi nchini humo kwa kuwahami na kuwafadhili wapiganaji wanaotaka kuuangusha utawala wa rais Bashar Al Assad.